• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ajibu ataja sababu zilizomuengua kikosi cha kwanza Simba

    (GMT+08:00) 2020-05-14 16:51:51

    Kiungo Mshambuliaji Wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa sababu kubwa ya kutokuwa kwenye kikosi cha kwanza ni matatizo ya kifamilia. Ajibu ameweka wazi kuwa awali chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroec alikuwa na nafasi kikosi cha kwanza ila mambo yalibadilika alipopata matatizo. Anasema mtoto wake aliumwa na kulazwa hospitali hivyo hakuweza kusafiri na timu kwa kuwa alikuwa anamuuguza, na pia alikuwa akiuguza majeraha yake wakati huo timu ya Simba ilienda kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na Lipuli kule Iringa, ambapo timu hiyo ilifanya vizuri, na inafahamika kuwa, timu inayofanya vizuri, si rahisi kubadilishwa. Na hiyo ndio sababu ya yeye kutokuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, kwani awali kabla ya matatizo hayo, alicheza mechi nyingi chini ya kocha Sven.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako