• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mchezaji wa Uturuki aua mtoto wake kisa hampendi

    (GMT+08:00) 2020-05-14 16:52:13

    Beki wa Klabu Bursa Yildirim Spor, Cevher Tokts raia wa Uturuki amekiri kumuua mtoto wake kwa kuwa alikuwa hampendi na kujisalimisha polisi. Tukio hilo, lilitokea Aprili 23, mwaka huu ambapo beki huyo alimpeleka mtoto wake huyo wa miaka mitano hospitali baada ya kuonyesha dalili za virusi vya corona. Lakini baadaye, mchezaji huyo aliwaambia wauguzi kuwa mtoto wake huyo wa kiume alikuwa na tatizo la kushindwa kupumua hivyo alipelekwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na kisha kufariki. Hata hivyo baada ya siku kaadha, mchezaji huyo alijipeleka polisi mwenyewe na kukiri amemua mtoto huyo kwa sababu alikuwa hampendi. Mchezaji huyo alikiri mwenyewe mbele ya polisi na kusema, mtoto alipolala, alichukua mto na kuweka kichwani na kumfumba mdomo kwa dakika 15 kwani alikuwa hampendi tangu alipozaliwa na ndiyo maana aliamua kumuua. Alimalizia kwa kusema hana tatizo lolote la akili na alifanya hivyo kwa kukusudia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako