• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wenye viwanda wakutana na kanuni kali katika sheria mpya iliyopendekezwa

    (GMT+08:00) 2020-05-14 19:52:03
    Kanuni mpya nchini Kenya zinapendekeza wenye viwanda vya kupakia na kutengeneza bidhaa nchini humu kusafisha uchafu kutoka kwa bidhaa zao baada ya kutumiwa na walaji.

    Kanuni za Uratibu na Usimamizi wa Mazingira 2020,zinalenga kuwafunga wazalishaji bidhaa katika taka zinazotokana na bidhaa zao baada ya wanunuzi kutumia bidhaa hizo.

    Katika rasimu ya kanuni hizo iliyotayarishwa na Wizara ya Mazingira na Misitu nchini Kenya ,mzalishaji atatwikwa jukumu la uchafu wa bidhaa zao,ikiwa ni pamoja na kukusanya,kutenganisha ,kutia dawa ,kwa ajili ya kuunda upya bidhaa za ufungaji.

    Wenye viwanda watalazimika kutambua na kurejesha upya taka zote zinazotoka katika viwanda vyao.

    Vilivyolengwa ni bidhaa za ufungaji,betri,mafuta,vyuma,bidhaa za plastiki na glasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako