• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafikiria kuuza mazao nje kwa njia ya mtandao

    (GMT+08:00) 2020-05-14 19:52:26

    Endapo ugonjwa wa virusi vya Corona utaendelea kwa muda mrefu, serikali ya Tanzania itatumia njia ya mtandao kuuza mazao nje ya nchi.

    Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.

    Hasunga alisema pia watawatumia mabalozi wa Tanzania walioko nchi mbalimbali ambao watatafuta wafanyabiashara wakubwa na kuingia nao mikataba ya ununuzi wa mazao nchini.

    Kuhusu kuwatumia mabalozi, Waziri Hasunga alisema watawapa mamlaka mabalozi kutafuta wateja na kuingia nao mikataba ya manunuzi moja kwa moja.

    Waziri Hasunga alisema matarajio ya wizara kwa mwaka ujao wa fedha ni kuhakikisha Tanzania inakuwa kinara wa uzalishaji wa chakula kwa nchi za Afrika Mashariki.

    Alisema kwa mwaka wa fedha ujao wameweka malengo ya kuzalisha tani 400,000 za pamba, kutoka tani 352,000 zilizozalishwa mwaka huu.

    Waziri Hasunga alisema kwenye zao la korosho wameweka malengo ya kuzalisha tani 350,000, chai tani 40,000, kahawa tani 90,000, miwa tani milioni 4.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako