• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waganda watumia $88m kuagiza vipodozi na manukato

    (GMT+08:00) 2020-05-14 19:52:47
    Waganda wametumia takriban Ush335bilioni ($88m) kuagiza vipodozi na manukato.

    Haya ni kwa mujibu wa Ripoti ya Wizara ya Fedha nchini humo.

    Kulingana na Ripoti hiyo,ambayo inaonyesha takwimu za kutokea Januari hadi Disemba 2019,Uganda ilitumia kiwango kikubwa cha fedha kwa bidhaa za urembo,mafuta ya kujipaka,na manukato.

    Chini ya kitengo hiki,kulingana na Ripoti hiyo,mchanganyiko wa bidhaa mbalimbali zinazotumika kama mali ghafi zimechukua sehemu kubwa ya vilivyoagizwa huku nchi hiyo ikiagiza bidhaa hizo zenye thamani ya Ush57bn ($15mn) katika kipindi hicho.

    Aidha Ripoti hiyo inaonyesha kuwa katika kipindi hicho,Ush45.6bn ($12m) zilitumiwa kuagiza bidhaa za urembo,ngozi na bidhaa za kutengeza kucha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako