• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: TP Mazembe yakanusha tetesi za kumsajili Mcameroon Villa Jean Makoun

  (GMT+08:00) 2020-05-15 08:20:05

  Klabu ya soka ya TP Mazembe ya nchini DR Congo, imekanusha tetesi za kumsajili kiungo wa zamani wa klabu za Lyon na Aston Villa Jean Makoun raia wa Cameroon. Kupitia taarifa yake TP Mazembe wamesema hakuna ukweli kuhusu tetesi hizo ambazo zimekuwa zikielezwa kupitia mitandao mbalimbali ya Cameroon na DRC. Taarifa hiyo imefafanua kuwa hawajamsajili na wala hawana mpango na Jean Makoun, hata hivyo imekiri kuwa ni mchezaji mzuri lakini imesema kikosi chao hakina uhitaji wa huduma yake kwasasa. Jean Makoun alifanya vizuri kwenye soka ya Ulaya akiwa na klabu ya Lyon kati ya mwaka 2008 na 2011 kisha Aston Villa kuanzia mwaka 2011 hadi 2013. Lakini pia amechezea vilabu tofauti tofauti vya Ulaya ikiwemo Lille ya Ufaransa na Olympiacos ya Ugiriki. Kwasasa Jean Makoun akiwa na umri wa miaka 36 hana klabu hivyo akisajiliwa atakuwa ni mchezaji huru na huenda timu isipate gharama kubwa kupata sahihi yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako