• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chakula kinauzika sokoni kuliko bidhaa nyinginezo

    (GMT+08:00) 2020-05-15 20:18:37
    Kufuatia kuendelea kuongezeka kwa idaadi ya maambukizo nchini Kenya wafanyabiashara wa chakula wanaonekana kujipatia faida kubwa zaidi wakati huu wa janga la Corona. Uchunguzi uliofanywa kwenye masoko mengi nchini Kenya unaonesha kuwa wafanyabiashara wengi wameamua kuuza bidhaa za kula.

    Hatua hiyo imetokana na biashara nyingi hasa zisizo za bidhaa za kula kudorora, athari zilizochangiwa na janga la corona ambalo limeathiri uchumi wa nchi na ulimwengu kwa jumla.

    Baadhi ya wafanyabiashara tuliozungumza nao wanasema wamelazimika kufunga maduka, taswira inayoonyesha namna Wakenya wamepoteza nafasi za kazi katika kampuni, mashirika mbalimbali na hata kazi za wenyewe kujiajiri. Waathirika wengi wamegeukia biashara ya bidhaa za kula kukidhi mahitaji ya kimsingi.Wengi wao wanasema awali walikuwa wakiuza bidhaa tofauti kama vile nguo, vifaa vya kieletroniki na viatu lakini sasa wamegeukia bidhaaza kula kutokana na kuongezeka kwa mahitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako