• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Hellen Obiri na Faith Kipyegon watarajia kurejea kwenye mbio wakiwa na nguvu na ari kubwa

  (GMT+08:00) 2020-05-19 08:46:26

  Hellen Obiri na Faith Kipyegon ni miongoni mwa Wakenya waliokuwa wafungue kampeni za Diamond League mjini Shanghai, China wikendi iliyopita kabla ya kivumbi hicho kuahirishwa hadi Septemba 19, 2020. Kipyegon ambaye ni bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 1,500 ana matarajio ya kurejea Shanghai kwa matao zaidi hasa ikizingatiwa kwamba ndiko alikowahi kuandikisha muda bora zaidi wa kibinafsi wa dakika 3:56.82 katika mbio hizo za mizunguko minne mwaka 2016 na kuandika historia ya mbio hizo. Ushindi wa Kipyegon katika kivumbi hicho unatarajiwa kumtia hamasa ya kutamba hata zaidi kwenye Olimpiki zitakazoandaliwa Tokyo, Japan 2021. Kwa upande wake, Obiri amekuwa akishiriki mazoezi makali kwa nia ya kuweka muda bora zaidi katika mbio za mita 5,000. Mtimkaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema kwamba angali na matarajio makubwa ya kujinyakulia dhahabu katika Olimpiki zijazo za Tokyo. Hata hivyo, Obiri anashikilia kwamba mabadiliko kwenye kalenda iliyotolewa majuzi na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) yatawapa wanariadha wengi ugumu wa kurejea katika hali zao bora zaidi kabla ya kivumbi cha kwanza cha Diamond League kuandaliwa jijini Olso, Norway mnamo Juni 11, 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako