• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Chelsea kutembeza mkwanja mrefu ili kujenga kikosi kipya msimu ujao

    (GMT+08:00) 2020-05-19 08:47:40

    Chelsea iliyo chini ya Kocha Mkuu Frank Lampard inapiga hesabu kupitisha panga la moto kwa wachezaji wake ili kujenga kikosi kipya msimu ujao. Licha ya hali kuwa tete kiuchumi kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vimeivuruga dunia Chelsea inapiga hesabu ndefu za kushusha majembe mapya. Miongoni mwa majina yanayotajwa sana ni pamoja na Jadon Sancho anayekipiga ndani ya Borussia Dortmund ambaye pia anawindwa na Manchester United. Majina ya nyota ambao panga linawahusu ni pamoja na Tiemoue Bakayoko anayekipiga Monaco kwa mkopo, Marcos Alonso, Emerson Palmieri, Michy Batashuayi na David Zappacosta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako