• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mhariri mkuu wa The Lancet adhihirisha makosa ya Rais Donald Trump wa Marekani kwenye barua yake kwa WHO

  (GMT+08:00) 2020-05-20 09:41:34

  Jarida maarufu la matibabu The Lancet limetoa taarifa ikidhihirisha makosa ya rais Donald Trump katika barua aliyoitoa kwa Shirika la Afya Duniani WHO.

  Kwenye barua hiyo rais Trump aliandika kuwa, uchunguzi wa serikali ya Marekani umetambua WHO ilipuuza kuwa "ripoti zinazoaminika ambazo zilitolewa na mashirika mbalimbali ikiwemo The Lancet mwanzoni mwa mwezi Desemba au mapema zaidi, kuhusu mlipuko wa virusi mjini Wuhan."

  Mhariri mkuu wa The Lancet Bw. Richard Horton, amesema rais Trump alifanya makosa kwenye barua hiyo, kwa sababu jarida hilo halikutoa ripoti kuhusu mlipuko wa virusi uliotokea mjini Wuhan au sehemu nyingine nchini China mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka 2019, na kwamba jarida hilo lilitoa ripoti ya kwanza tarehe 24 Januari mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako