• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Edward Rombo ateuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Kenya Rugby League

    (GMT+08:00) 2020-05-20 11:03:01

    Mwanaraga Edward Rombo ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Kenya Rugby League. Rombo ataongoza programu ya timu ya taifa na kushirikiana na wakfu wa Giving Rugby Foundation kupiga jeki juhudi za benchi la kiufundi na Shirikisho la Raga la Kenya katika kukuza vipaji miongoni mwa wanaraga nchini Kenya. Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, anajivunia takriban miaka 30 ya uchezaji na ukufunzi katika Ligi na Shirikisho la Raga. Ni Mkenya wa kwanza kuwahi kucheza kikosi cha Leeds Rugby, Dewsbury na Featherstone Rovers, Uingereza katika miaka ya 90. Rombo ambaye ni fowadi, alicheza misimu mingi ya kuridhisha katika Raga ya Shirikisho hasa ikizingatiwa kwamba aliwahi kuwaongoza Mean Machine kujizolea ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya Cup mnamo 1989 na 1990. Amewahi pia kuchezea klabu za Watembezi Pacesetters na Barclays RFC. Rombo, anayemiliki kampuni ya masuala ya uanasheria ya Rombo and Co Advocates, amewahi pia kuwa kocha wa kikosi cha Mwamba RFC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako