Kahwa aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani ambayo hufanyika Mei 20 kila mwaka huk kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "Vipimo katika Biashara za Kimataifa".
Bi Kahwa alisema kuwa nchi ya viwanda inajengwa kwa kuzingatia vipimo sahihi kwa kuangalia malighafi mpaka mali inayozalishwa.
Aidha Kahwa aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwawezesha kwa kiasi kikubwa kwani mpaka sasa wana magari ya kutosha ,watumishi wameongezwa ,pia wamefanikiwa kupata kituo kikubwa kwa ajili ya kupimia magari ya mafuta.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |