• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Zanzibar yaweka mikakati ya kuimarisha utalii katika kisiwa cha Pemba

  (GMT+08:00) 2020-05-21 19:33:57
  Serikali ya Zanzibar imesema imejipanga kuhakikisha sekta ya utalii inaimarika katika kisiwa cha Pemba na kukuza uchumi wa Taifa na pato la wananchi kwa ujumla.

  Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari,Utalii,na Mambo ya Kale,Mahmoud Thabit Kombo,wakati akifanya majumuisho na kujibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi jana waliochangia bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2020-2021.

  Alisema tayari serikali imetangaza utalii kwa wote kwa lengo la kuwanufaisha wananchi na kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

  Alisema serikali inanuia kuliimarisha eneo la Kaskazini ya Micheweni kuwa moja ya kivutio cha utalii kwa kujenga hoteli kubwa za kitalii.

  Alikiri kuwa sekta ya utalii imechelewa kuimarika katika kisiwa hicho kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ukosefu wa miundombinu ya barabara na umeme.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako