• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Fedha za GEP kusaidia watoto walio hatarini barani Afrika kuendelea na masomo

  (GMT+08:00) 2020-05-21 20:17:52

  Uhusiano wa Kimataifa kuhusu Elimu (GEP) umetangaza mchango wa awali wa dola za kimarekani milioni 60 za mkopo kusaidia watoto milioni 30.5 katika nchi za Ghana, Malawi, Msumbiji, Rwanda na Zambia kuendelea na masomo.

  Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa GEP Alice jijini Lagos, Nigeria imesema, mkopo huo utasaidia nchi hizo kuhakikisha watoto wa kike na wa kiume wanaendelea na masomo kupitia mpango wa masomo huria yanayomfikia kila mmoja, na kuunga mkono walimu na wanafunzi kuhakikisha kuwa watoto walio hatarini zaidi hawaachwi nyuma.

  Amesema mkopo huo utasaidia juhudi za serikali katika nchi husika kuhakikisha kuwa watoto wanaendelea kusoma wakati shule zimefungwa, kuunga mkono walimu na wazazi kutoa masomo ya ubora wa juu majumbani na kukabiliana na mahitaji ya watoto ya kisaikolojia na kijamii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako