• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kupunguza orodha ya sekta zilizozuiliwa kwa uwekezaji kutoka nje

  (GMT+08:00) 2020-05-22 10:52:12

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo amesema China itapunguza zaidi orodha ya sekta zilizozuiliwa kwa uwekezaji kutoka nje kuingia kwenye soko la China, kuweka orodha ya sekta zilizozuiliwa kwa huduma na biashara nje ya nchi, na kuyapatia maeneo ya majaribio ya biashara huria haki zaidi ya kujiamulia juu ya mageuzi na kufungua mlango.

  Ameongeza kuwa China inalinda kithabiti mfumo wa biashara ya pande nyingi, na kushiriki kwenye mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani. Pia inahimiza kusaini makubaliano ya ushirikiano wa wenzi wa kiuchumi wa pande zote wa kikanda RCEP, kuhimiza mazungumzo ya biashara huria kati ya China, Japan na Korea Kusini, na kutekeleza kwa pamoja makubalilano ya kibiashara ya awamu ya kwanza kati ya China na Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako