• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wa afya wa China na Sudan wabadilishana uzoefu wa kupambana na COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-05-22 16:30:16

  Maofisa wa wizara ya afya na wataalamu wa matibabu kutoka China na Sudan jana walihudhuria kongamano la kimataifa la MedixChange kwa kupitia mtandao wa inteneti wakibadilishana uzoefu wa tiba na ujuzi kuhusu kukinga virusi vya Corona na kuwatibu wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo.

  Akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano hilo, Naibu waziri wa afya wa Sudan Bibi Sara Abdelazim Hassanain amesema kubadilishana ujuzi wa kitaalam ni muhimu sana, haswa kwa nchi zenye mapato ya chini na dhaifu ambazo zinakabiliana na changamoto kubwa kutokana na virusi hivyo.

  Kongamano hilo lililoandaliwa na wizara ya afya ya Sudan na Hospitali ya Pili ya Taasisi ya Matibabu ya chuo kikuu cha Zhejiang (SAHZU) cha China, lilihudhuriwa na washiriki zaidi ya 80 wakiwemo wataalam wa matibabu na madaktari.

  Mkuu wa SAHZU Bw. Wang Jian'an alifahamisha wenzao wa Sudan uzoefu wa usimamizi wa hospitali , hatua za kinga kwa wafanyakazi wa afya na matibabu na usimamizi wa wagonjwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako