• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema kuchochea mzozo katika uhusiano wake na Afrika ni kitendo cha kujidhalilisha

  (GMT+08:00) 2020-05-22 18:52:53

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, njama ya kuchochea mzozo katika uhusiano wake na nchi za Afrika ni kitendo cha kujidhalilisha.

  Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni, jopo la washauri bingwa la Marekani Heritage Foundation kuripoti kuwa pengine majengo ya kiserikali barani Afrika ni mahali pa China kufanya shughuli za ujasusi. Zhao Lijian amesema, ripoti hiyo haina ukweli na imejaa upendeleo wa kiitikadi, na ni uchochezi na kurudia shutuma isiyo na msingi ya "China kufanya ujasusi katika makao mkuu ya Umoja wa Afrika", ambayo imekosolewa na viongozi wa nchi nyingi za Afrika. Zhao amesema ikiwa rafiki, mwenzi na ndugu mzuri wa nchi za Afrika, China siku zote imefanya ushirikiano wa kivitendo na nchi za Afrika, na kujenga miundombinu mingi katika nchi hizo, ambayo imewaletea manufaa halisi watu wa Afrika na kuandaa mazingira kwa nchi nyingine kufanya ushirikiano na nchi za Afrika.

  Zhao ametoa wito kwa jopo la washauri bingwa kama hilo kutumia muda mwingi kufanya mambo ya kuzinufaisha kihalisia nchi za Afrika badala ya kusambaza uvumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako