• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ndoto ya David Luiz nikumalizia soka yake na klabu ya Benfica ya Ureno

    (GMT+08:00) 2020-05-25 08:11:14

    Wakati mkataba wake na Arsena ukibakisha mwaka mmoja, beki Mbrazil David Luiz (33) amefichua kuwa hana mpango wa kustaafia soka klabuni hapo. Badala yake Luiz amedai kuwa angependa amalizie soka ya ushindani akiwa anachezea klabu yake ya moyoni Benfica ya Ureno ambayo ndio ilichangia kwa kiasi kumfanya awe nyota mkubwa hivi sasa. Beki huyo alisema kuwa hawezi kuficha mahaba aliyonayo kwa Benfica na anatamani kurejea tena kwenye klabu hiyo aliyoichezea kuanzia 2007 hadi 2011 baada ya kujiunga nayo akitokea Vitoria ya Brazil. Luiz ametoa kauli hiyo licha ya hamu ya kocha wa Arsenal Mikel Arteta kutamani kuendelea kubaki naye klabuni akikoshwa na sifa za uongozi alizonazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako