• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Bayern Munich na Borussia Dortmund bado zaendelea kusuguana

    (GMT+08:00) 2020-05-25 08:11:38

    Ushindi wa timu za Bayern Munich na Borussia Dortmund katika mechi za Ligi Kuu ya Ujerumani 'Bundesliga' Jumamosi, umezidi kunogesha vita vya kuwania ubingwa baina yao. Matokeo hayo yamefanya pengo la pointi nne (4) lililopo baina ya vinara Bayern na washindi wa pili, Dortmund kuendelea kubaki vilevile huku ligi hiyo ikibakisha raundi saba kabla ya kufikia tamati. Jijini Munich katika Uwanja wa Allianz Arena, wenyeji Bayern Munich waliangusha kipigo kikali cha mabao 5-2 kwenda kwa Eintracht Frankfurt kilichowafanya wazidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi wakifikisha pointi 61. Robert Lewandowski anayeongoza mbio za ufungaji bora katika ligi hiyo, alipachika moja kati ya mabao hayo matano ya Bayern huku mengine manne yakifungwa na Leon Goretzka, Thomas Mueller, Alphonso Davies na moja la kujifunga la Martin Hinteregger. Bao hilo moja ambalo Lewandowsski amepachika lilifanya afikishe mabao 27 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa zawadi ya kiatu cha dhahabu kwa mfungaji bora wa ligi hiyo msimu huu. Mabao mawili ya Frankfurt yalipachikwa na Hinteregger Jijini Wolfsburg katika dimba la Volkswagen Arena, wenyeji Wolfsburg walijikuta kichwa chini mbele ya Borussia Dortmund baada ya kuchapwa mabao 2-0. Mabao hayo yote yaliyofungwa na mabeki wa pembeni Raphael Guerreiro na Achraf Hakimi yalitosha kuifanya Dortmund ifikishe pointi 57 na kuendelea kukimbizana na Bayern Munich katika mbio za ubingwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako