• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yanga kumtumia tiketi kocha wake Mbelgiji Luc Eymael na msaidizi wake

    (GMT+08:00) 2020-05-25 08:12:02

    Uongozi wa Yanga umepanga kuwarejesha makocha wake, Mbelgiji, Luc Eymael na msaidizi wake raia wa Afrika Kusini, Riedoh Berdien waliopo nje ya nchi baada ya Serikali kutangaza kurejesha michezo ikiwemo Ligi Kuu Bara kuanzia Juni Mosi, mwaka huu. Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema,wamepanga kuwatumia tiketi za ndege makocha hao haraka baada ya Rais kutangaza kuruhusu ndege kutoka mataifa mengine kuanza kuingia nchini humo. Aliongeza kuwa hivi sasa wanaangalia ndege gani itakayomfaa kocha huyo kumfikisha Tanzania ili kuungana na kikosi cha timu hiyo kitakachokuwa chini ya Charles Mkwasa. Eymael naye alipotafutwa kuzungumzia hilo alisema anashukuru kusikia ndege zimeanza kuruhusiwa kuingia Tanzania, na binafsi yake amefarijika na mipango ya safari ikikamilika atarudi kuendelea na ligi, akiwa na lengo la kuipa mafanikio klabu yake ya Yanga kwa kushika nafasi za juu katika msimamo wa ligi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako