• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ataka kuinua uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza

    (GMT+08:00) 2020-05-25 08:48:52

    Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuongeza uwezo wa kusimamia, kutoa tahadhari na kuitikia hali ya dharura ya magonjwa ya mlipuko.

    Rais Xi amesema hayo aliposhiriki katika mjadala wa jopo la wajumbe wa mkoa wa Hubei wanaohudhuria mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China unaoendelea hapa Beijing.

    Rais Xi amesisitiza kuufanyia mageuzi mfumo wa kukinga na kudhibiti magonjwa, kuboresha huduma za afya ya umma, na kukamilisha utaratibu wa bima ya afya na kutoa usaidizi kwa watu wenye magonjwa makubwa. Pia ametaka kasi ya kujenga mfumo wa sheria na taratibu kuhusu afya ya umma iongezwe, na utaratibu wa utekelezaji wa sheria kuhusu kinga na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza ukamilishwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako