Alhamisi wiki hii, Tanzania inatarajia kupokea ndege nyingi zaidi zikiwamo za watalii. Awali, Rais Magufuli alidokeza kwamba, watanzania watarajie watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.
Tayari mashirika kadhaa ya ndege yameratibiwa safari za kusafirisha vyakula na mizigo mingine kutoka Tanzania hadi mataifa mengine.
Aprili, 11, mwaka huu, Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania (TCAA), yalifuta safari zote za ndege za abiria kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Hata hivyo, kutokana na tathmini ya mwenendo wa virusi hivi, Mei 18 mwaka huu, serikali ya Tanzania ilitangaza kufunguliwa kwa usafiri wa anga ya Tanzania kwa ndege zote za kibiashara, misaada, kidiplomasia, za dharura na ndege maalum.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |