• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Arsene Wenger aapa hatarejea Arsenal

    (GMT+08:00) 2020-05-25 17:11:01

    Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amefichua kuwa hana nia yoyote ya kurejea ugani Emirates. Mfaransa huyo alijiuzulu kutoka kwa wadhifa wake kama kocha mkuu wa Gunners msimu wa mwaka 2018 baada ya kuwanoa kwa misimu 22. Hata hivyo, Mfaransa huyo alisema hana mpango wowote wa kurejea Emirates hata kama mtazamaji licha ya kupendekezewa nyadhifa kadhaa. Wakati wa utawala wake, Wenger alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu katika klabu hiyo na kisha kuwa kocha pekee ambaye hakuwahi kupoteza mechi yoyote kampeni mzima. Nguli huyo wa miaka 70 ameonyesha kufurahishwa na Liverpool kushindwa kuweka rekodi hiyo aliyopata msimu wa 2003-04. Wenger alionyesha kupata afueni baada ya Watford kuifunga Liverpool kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu kwenye mchezo uliomalizika kwa mabao 3-0 kwa Reds mwezi Februari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako