• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kuboresha uhusiano kati yake na Marekani kunalingana na maslahi ya watu wa China na Marekani na dunia nzima

    (GMT+08:00) 2020-05-25 18:33:32
    Mkutano wa tatu wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China umeandaa mkutano na waandishi wa habari kuhusu "Sera za mambo ya kidiplomasia za China na uhusiano na nchi za nje," wakati uhusiano kati ya China na Marekani ukiwa katika kipindi muhimu. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameeleza kuwa, China na Marekani zinaweza kufanya ushirikiano licha ya tofauti nyingi zilizopo kati ya pande hizo mbili. Wajumbe wengi wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wanaona kuwa, kusikilizana kwa amani na kunufaishana kunalingana na maslahi za nchi hizo mbili, na kupata maendeleo ya pamoja kwa China na Marekani kunalingana na maslahi ya dunia nzima.
    Akizungumzia uhusiano kati ya China na Marekani, Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa Kituo cha utafiti kuhusu mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Jia Qingguo anasema:
    "Mlipuko wa virusi vya Corona ungesaidia nchi hizo mbili kuacha migongano iliyokuwepo katI ya pande hizo mbili na kupambana kwa pamoja janga hili. Lakini ni bahati mbaya kuwa ushirikiano wa nchi hizo mbili hauendelei vizuri."
    Kwa maoni ya Bw. Jiang Qingguo, uhusiano kati ya China na Marekani ulikuwa umebadilika kiasi kabla ya kulipuka kwa janga hili, na kuenea kwa virusi vya Corona kumekuwa kisigizio kwa baadhi ya wanasiasa wa Marekani kuipaka matope China. Anasema, hivi sasa changamoto zote zinazoikabili dunia inategemea uratibu kati ya nchi mbili kubwa za China na Marekani, na kutokana na mtizamo wa muda mrefu katika siku za baadaye, bado kuna msingi kwa nchi hizo mbili kubwa duniani kufanya ushirikiano.
    Mtafiti wa Taasisi ya utafiti wa mambo ya Marekani katika Chuo cha jamii na sayansi cha China Bibi Zhao Mei vilevile anaona kuwa, kutegemeana na kupata maendeleo kwa pamoja kati ya China na Marekani kutalingana na maslahi ya nchi hizo mbili na za dunia. Anasema:
    "Katika miaka 40 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani, mawasiliano ya watu, mambo ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakiimarishwa na ni vigumu kuyazuia, na ni njia kuu kwa pande hizo mbili kutegemeana, na inatakiwa kufanya juhudi za kuhimiza ushirikiano wenye utulivu kati pande hizo mbili."
    Pia amependekeza kuwa, ili kukabiliana na mashambulizi ya baadhi ya wanasiasa wa Marekani dhidi ya China, China inatakiwa kudumisha mikakati yake na kushughulikia vizuri mambo yake yenyewe kadiri iwezavyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako