• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wuhan yafanya vipimo milioni 6.5 vya virusi vya Corona katika siku 10

    (GMT+08:00) 2020-05-25 18:48:32

    Mji wa Wuhan ulioko katikati ya China umefanya vipimo 6,574,093 vya maambukizi ya virusi vya Corona kati ya tarehe 14 na 23 mwezi huu.

    Kamati ya Afya ya mji wa Wuhan imesema, Jumamosi pekee, mji huo ulipima watu 1,146,156, ikiwa ni mara 15 zaidi ya idadi ya tarehe 14 mwezi huu, wakati mji huo ulipoanza kampeni ya upimaji katika mji wote. Kampeni hiyo inalenga kufahamu idadi ya kesi zenye maambukizi lakini hazionyeshi dalili licha ya kuwa na virusi vya Corona.

    Uamuzi wa kufanya vipimo katika eneo kubwa zaidi pamoja na kwa wale ambao awali hawakufanyiwa vipimo ulifikiwa wakati Wuhan ilipoendelea kuripoti kesi za maambukizi kwa watu wasio na dalili, hivyo kuongeza wasiwasi kwa jamii wakati Wuhan ikifungua tena viwanda, shule na biashara.

    Kamati hiyo imesema, vipimo hivyo ni vya hiari na havilipiwi gharama yoyote. Kipaumbele kitawekwa kwa maeneo ya makazi ambayo awali yaliripoti maambukizi na pia katika majengo ya zamani yenye idadi kubwa ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako