• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya wajumbe wa kudumu wa bunge la umma la China yawasilisha ripoti ya kazi katika mkutano wa mwaka wa bunge hilo

    (GMT+08:00) 2020-05-25 20:48:05

    Kamati ya wajumbe wa kudumu ya bunge hilo imewasilisha ripoti ya kazi ili iweze kujadiliwa katika mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China unaoendelea hapa Beijing.

    Ripoti hiyo imesisitiza kuendelea kuzitawala Hong Kong na Macau kwa kufuata sheria, kulinda utaratibu wa katiba uliowekwa na sheria ya msingi, kuboresha mfumo wa ufafanuzi wa kamati hiyo kwa sheria ya msingi, na kujenga mfumo wa sheria na wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa mikoa yenye utawala maalumu kutoka upande wa taifa.

    Ripoti hiyo pia imesema, mwaka huu kamati hiyo itaweka kipaumbele katika sheria za afya, sheria ya hifadhi ya wanyamapori, sheria ya kukinga maradhi ya kuambukiza, pia kamati hiyo itaendelea kufuatilia usimamizi wa majukumu makubwa ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China.

    Mbali na hayo, ripoti hiyo imesema, Bunge litaendelea kuimarisha mawasiliano na viongozi wa nchi za nje, kuhimiza kwa utulivu mawasiliano ya mifumo na kushiriki ushirikiano wa pande mbalimbali kati ya mabunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako