• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China asema jambo unalosema limenipa kumbukumbu nyingi

    (GMT+08:00) 2020-05-25 20:48:56

    Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mjadala wa ujumbe wa mkoa wa Hubei unaohudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China. Wakati mkuu wa hospitali ya Taihe ya Hubei, ambaye pia ni mjumbe wa bunge hilo Bw. Luo Jie alipotoa hotuba, rais Xi amesema alimuona kwenye televisheni akieleza jinsi ya kumtibu mzee mwenye umri wa miaka 87, na kumpa kumbukumbu nyingi.

    Baada ya mlipuko wa virusi vya Corona, rais Xi amesisitiza mara nyingi kutumia nguvu zote kumtibu kila mgonjwa. Zaidi ya timu 340 za madaktari kote nchini na wafanyakazi zaidi ya elfu 42 wa afya walienda kuusaidia mkoa wa Hubei kupambana na mlipuko wa virusi hivyo. Wagonjwa zaidi ya elfu 3,600 wenye umri wa miaka zaidi ya 80 wametibiwa, kati yao 7 wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako