• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TANZIA: Katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga Lawrence Mwalusako afariki dunia

    (GMT+08:00) 2020-05-26 08:28:12

    Aliyewahi kuwa mchezaji na Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Lawrence Mwalusako amefariki dunia jana Asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa hiyo imethibitishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Tanzania, Mussa Kisoki ambapo amesema kuwa Mwalusako alikuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji. Katika maisha yake ya soka, Lawrence Mwalusako alianzia katika klabu ya Waziri Mkuu ya Dodoma kisha akajiunga na Yanga ambapo baada ya kustaafu alikuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo. Mussa Kisoki amemzungumzia Mwalusako kuwa ni mtu mcheshi tangu alipokuwa mchezaji na hata katika uongozi wake, pia alisifika kwa kusimamia kwa umakini mipango mbalimbali, akitaja mfano kuwa alikuwa hana masihara hata katika masuala ya mazoezi ya klabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako