• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Hatma ya Alphonce Simbu na Failuna Abdi Olimpiki yaeleweka

    (GMT+08:00) 2020-05-26 08:28:37

    Shirikisho la Riadha la dunia (WA) limewashusha presha wanariadha nyota wa Tanzania wa mbio ndefu za barabarani (marathoni), Alphonce Simbu na Failuna Abdi juu ya hatma yao ya kushiriki Olimpiki msimu ujao. Simbu na Failuna walikuwa mguu ndani mguu nje juu ya viwango vyao baada ya michezo hiyo iliyokuwa ianze Julai kuahirishwa hadi 2021 kutokana na janga la corona. Uamuzi wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) kuahirisha michezo hiyo uliwaweka gizani wanariadha hao pekee Tanzania waliokuwa wamefuzu kushiriki Olimpiki kabla ya kuahirishwa endapo wataendelea na viwango vya awali au wataanza upya, huku IOC ikitaka vyama vya kitaifa kuwasiliana na mashirikisho ya michezo yao ya kimataifa ili kujua mchakato wa kufuzu ukoje. Hata hivyo msimano wa WA, chini ya rais wake, Sebastian Coe umeeleza kuwa wanariadha waliokuwa wamefuzu kabla michezo hiyo kuahirishwa watashiriki Olimpiki 2021 kule Japan kwa viwango vile vile vya awali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako