• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Naomi Osaka amzidi Serena kwa kupokea mkwanja mrefu zaidi

    (GMT+08:00) 2020-05-26 08:28:59

    Nyota wa kike wa mchezo wa tenisi, Naomi Osaka amempiku mkongwe Serena Williams kwa kuwa mchezaji aliyepiga pesa nyingi zaidi kwa mwaka uliopita. Kwa mujibu wa Jarida la Forbes ambalo ni la kibiashara, nyota huyo wa tenisi mwenye umri wa miaka 22 kutoka Japan, ameweka kibindoni Pauni milioni 30.7 ndani ya miezi 12 iliyopita kutokana na zawadi na malipo mengine, ikiwa ni zaidi ya Pauni milioni 1.1 alizovuna Serena. Kiwango hicho kinazidi pia kile alichovuna Maria Sharapova mwaka 2015 cha Pauni milioni 24.4 kilichokuwa kikiweka rekodi kwamba ni kikubwa zaidi kuwahi kukusanywa na mcheza tenisi wa kike ndani ya mwaka mmoja. Osaka anashika namba 29 kwenye orodha ya jumla ya wakali waliovuna pesa nyingi ndani ya mwaka mmoja kwa wanamichezo 100, huku Serena akishika namba 33. Serena, 38, ambaye ni Mmarekani alikuwa akiongoza kwa kuvuna pesa nyingi kwa upande wa wanawake karibu kila mwaka kwa kipindi cha miaka minne iliyopita. Mwaka 2018, Naomi alimchapa Serena kwenye michuano ya Wazi ya Marekani na kubeba taji lake la kwanza la Grand Slam la mchezo wa tenisi kwa wanawake kabla ya kwenda kubeba taji la michuano ya Wazi ya Australia miezi mitano baadaye. Kwa sasa Naomi anashika namba 10 katika viwango vya ubora wa tenisi kwa upande wa wanawake duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako