• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji wa ubalozi wa China nchini Uingereza apinga kauli ya Christopher Francis Patten kuhusu Hongkong

    (GMT+08:00) 2020-05-26 09:50:45

    Msemaji wa ubalozi wa China nchini Uingereza amewakosoa wanasiasa wa nchi za magharibi akiwemo aliyekuwa gavana wa Hongkong Christopher Francis Patten kuhusu Hongkong.

    Msemaji huyu amesema baada ya mkutano wa 3 wa awamu ya 13 ya bunge la umma la China kutangaza kupitisha uamuzi wa kujenga na kukamilisha mfumo wa kisheria na taratibu za utekelezaji kuhusu mkoa maalumu wa kujiendesha wa Hongkong kulinda usalama wa taifa, wanasiasa wa Uingereza pamoja na wanasiasa wengine wa nchi za magharibi walichafua mambo ya Hongkong, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, kitendo ambacho China inakipinga kithabiti.

    Amesisitiza kuwa mambo ya Hongkong ni mambo ya ndani ya China, hayaruhusiwi kuingiliwa na nchi za nje. Kulinda usalama wa taifa ni mamlaka ya serikali kuu, na pia ni kiini na msingi wa sera ya "nchi moja, mifumo miwili".

    Pia amsema uamuzi huo unalenga vitendo vichache vinavyohujumu usalama wa China, si kama tu hautaathiri haki na uhuru wa wakazi wa Hongkong, bali utaweka mazingira salama ambayo haki halali na uhuru wa wakazi wa Hongkong vitaweza kutekelezwa vizuri zaidi. Uingereza haina mamlaka, haki ya usimamizi kwa Hongkong baada ya kurudi China, nchi yeyote haiwezi kuingilia kati mambo ya Hongkong na mambo ya ndani ya China kwa kisingizio cha "taarifa ya pamoja ya China na Uingereza".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako