• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Mafunzo ya bure ya saikolojia kwa wachezaji wa raga wa Kenya wakati huu wa janga la Covid-19

    (GMT+08:00) 2020-05-26 16:27:57

    Wachezaji wa raga wa Kenya wameanza Jumatatu kupokea ushauri wa kisaikolojia unaolenga kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa kuchukulia afya ya kiakili kwa uzito mkubwa wakati huu mgumu wa janga la virusi vya corona. Wanasaikolojia Rowena Tirop na Kanyali Ilako wameamua kutoa huduma hizo bila malipo ili wachezaji na makocha waweze kuimarisha viwango vyao vya utendakazi na afya yao ya kiakili kwa jumla. Tirop, ambaye ni mwanasaikolojia wa masuala ya michezo na mazoezi anasema, mlipuko huo umesababisha tabia za wachezaji kukaa tu badala ya kutumia nguvu zao mazoezini ambapo wamezoea., jambo lililochangia kuongezeka kwa magonjwa ya kiakili kama mtu kuwa na wasiwasi kila mara, kukosa utulivu, kukasirika ovyoovyo na kuwa na mabadiliko ya sununu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako