• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FKF, FIFA waafikiana jinsi Amrouche atakavyolipwa zaidi ya Sh109 milioni

    (GMT+08:00) 2020-05-26 16:28:16

    Hatimaye timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars sasa itashiriki mchujo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar baada ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kuafikiana na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu jinsi ambavyo zaidi ya Sh109 milioni zinazodaiwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Adel Amrouche, zitalipwa. Mwishoni mwa wiki jana, Nick Mwendwa ambaye ni Rais wa FKF, alisisitiza kwamba Kenya imeepuka adhabu kali ya FIFA ambayo vinginevyo, ingeshuhudia Harambee Stars wakitupwa nje ya michuano hiyo ya kuwania tiketi ya kuelekea Qatar. Awali, FIFA ilitarajiwa kuelekeza fedha za maendeleo ya soka ambazo Kenya hupokezwa kila mwaka kumlipa Amrouche; kocha mzawa wa Ubelgiji na raia wa Algeria ambaye kwa sasa anadhibiti mikoba ya timu ya taifa ya Botswana. FIFA iliwahi kuwapiga Zimbabwe marufuku ya kushiriki mchujo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2018 nchini Urusi kwa kosa la kukiuka masharti ya kandarasi na kumnyima haki mkufunzi mzawa wa Brazil, Jose Claudinei 'Valinhos' Georgino walipompiga kalamu mnamo Machi 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako