• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Borussia Dortmund yaalika Bayern Munich

    (GMT+08:00) 2020-05-26 16:28:32

    Vita vya ubabe kati ya chipukizi Erling Haaland na kigogo Robert Lewandowski vitatarajiwa kutawala leo Jumanne uwanjani Signal Iduna Park wakati nyota hao wawili watakapokutana kwa mara ya kwanza katika gozi la Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga). Haaland ambaye ni mzawa wa Norway ataongoza safu ya mbele ya Dortmund huku Lewandowski ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Poland akitazamiwa kuwa tegemeo la Bayern Munich ambao kwa sasa wako kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa alama 61, nne zaidi kuliko Dortmund ambao ni wa pili. Mabao 10 ya hadi kufikia sasa ambayo yamefungwa na Haaland katika Bundesliga yamesaidia Dortmund kutia kapuni jumla ya alama 27 kutokana na mechi 10 zilizopita mwaka 2020. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 alicheka na nyavu katika ushindi wa 4-0 uliosajiliwa na Dortmund dhidi ya Schalke wiki moja iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako