• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jaribio la wanasiasa wa Marekani la kuingilia kati mambo ya Hong Kong halitafanikiwa

    (GMT+08:00) 2020-05-26 19:26:12

    Baada ya Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China kutangaza kuuhusisha "ujenzi wa Mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa nchi katika mkoa wenye umaalumu wa Hongkong", wanasiasa wa nchi za magharibi akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo, wanadai kuwa hatua hiyo ya China itaifanya Hongkong kupoteza haki yake ya kujitawala, na kutishia kuiwekea China vikwazo.

    Lakini huu sio ukweli. Hong Kong ikiwa sehemu ya ardhi ya China, kuanzisha sheria ya usalama wa nchi mkoani humo kunafuata kanuni za kimataifa, na ni maslahi kuu kwa nchi zote duniani kulinda usalama wa nchi. Marekani yenyewe ina sheria mbalimbali zinazohusu maslahi ya usalama wa nchi, zikiwemo Sheria ya Usalama wa Nchi, Sheria ya Upelelezi, na serikali ya nchi hiyo siku zote inatoa kipaumbele cha usalama wa nchi.

    Kauli hizo za baadhi ya wanasiasa wa Marekani zimeonesha kuwa, hazilengi kufuatilia maslahi ya Hong Kong, bali wanachotaka ni kuivuruga Hong Kong, na kuhamisha ufuatiliaji wa wananchi wake juu ya kushindwa kwa mapambano dhidi ya virusi vya Corona, na kuzuia maendeleo ya China kwa kutumia fursa ya vurugu za Hongkong.

    Hongkong ikiwa mkoa wenye utawala maalumu wa China, uamuzi wa serikali ya China wa kujenga mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa nchi mkoani humo kuna fuata kanuni za kimataifa. Baada ya Hong Kong kurudi China, serikali kuu iliuidhinisha mkoa huo kutunga sheria za kulinda usalama wa nchi kwa kufuata kifungu No.23 cha sheria ya kimsingi ya Hongkong, lakini katika miaka 23 iliyopita, utaratibu unaohusika bado haujakamilika, hali ambayo imeisababisha Hongkong kuwa "eneo lisilo na ulinzi" ambayo ni nadra kuonekana katika sekta ya usalama wa nchi duniani.

    Wachambuzi wengi wa mkoa wa Hongkong wameeleza kuwa, uamuzi huo wa Bunge la Umma la China unalenga kupambana na vitendo vya nchi chache vya kudhuru vibaya usalama wa nchi. Utaratibu wa kutunga sheria utaanzishwa baada ya kupitishwa kwa uamuzi huo, hatua ambayo itaifanya Hongkong iwe na utaratibu kamili wa sheria, utaratibu wenye utulivu zaidi wa kijamii, na kuweka mazingira mazuri zaidi ya sheria na biashara, hali ambayo itasaidia makampuni ya nchi mbalimbali duniani kupata maendeleo mazuri zaidi mkoani Hongkong.

    Nia ya serikali ya China katika kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi haitabadilika, nia ya China ya kutekeleza sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" haitabadilika, na nia thabiti ya kupinga nguvu za nje kuingilia kati mambo ya Hongkong haitabadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako