• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Olympic Lyon kuishtaki FFF kwa kumaliza msimu na kuipa ubingwa PSG

    (GMT+08:00) 2020-05-27 08:32:34

    Klabu ya Olympic Lyon ya Ufaransa imeripotiwa kuanza ushindani wa kisheria na Shirikisho la soka Ufaransa (FFF) kufuatia uamuzi wao wa kumaliza msimu 2019/20 na kuitangaza PSG kama Bingwa. Lyon watapeleka kesi hiyo katika Mahakama za juu za Ufaransa, ikizingatiwa msimu huo umemalizika na msimamo kutambulika wao wakiwa nafasi ya 7 hivyo wanakosa hata nafasi ya kucheza Europa League. Ligue 1 na Ligue 2 Ufaransa zilimalizwa April huku Legue 1 ikiwa zimesalia mechi 10 kumalizia msimu kitu ambacho Lyon kinawaumiza na kulalamika kuwa klabu zitapoteza mapato ya karibia euro milioni 900. Rais wa klabu ya Lyon Jean-Michel Aulas ndio anaongoza malalamiko hayo na tayari ameshaongea na mamlaka husika akipeleka malalamiko yao Mahakamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako