• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa tatu wa China na Afrika kuhusu kinga na tiba ya COVID-19 wafanyika kwa njia ya video

    (GMT+08:00) 2020-05-27 09:55:37

    Mkutano wa tatu wa "Mawasiliano kati ya China na Afrika, Kushirikiana Kukabiliana na COVID-19" unaoandaliwa na Kamati ya Afya ya Taifa ya China na wizara ya mambo ya nje ya China umefanyika kwa njia ya mtandao wa Internet, na kushirikisha maofisa na wataalam kutoka China na nchi karibu 20 za Afrika na wajumbe wa Shirika la Afya Duniani WHO katika nchi hizo.

    Kwenye mkutano huo, wataalam wa China wamejulisha uzoefu wa kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, namna ya kugundua na kushughulikia wagonjwa wasio na dalili, na njia ya kupima virusi hivyo kwenye maabara. Aidha wamejibu zaidi ya maswali 40 ya washiriki kutoka Afrika.

    Wataalam wa Afrika wamepongeza kufanyika kwa mkutano huo, na kusema maswali yao yamejibiwa vya kutosha, na wanatarajia kushiriki kwenye mkutano ujao, ili kuendelea kujifunza uzoefu wa China katika kukabiliana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako