• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Bayern Munich wapiga wenyeji Borussia Dortmund 1-0

    (GMT+08:00) 2020-05-27 15:45:27

    Bayern Munich walianza kunusia ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kwa mara ya nane mfululizo msimu huu baada ya kuwazamisha Borussia Dortmund 1-0 uwanjani Signal Park Iduna. Wakinolewa na kocha wa sasa wa Liverpool, Jurgen Klopp, Dortmund walitawazwa mabingwa wa Bundesliga mnamo 2010-11 na 2011-12, na tangu wakati huo, Bayern wamekuwa wakijivunia umaarufu mkubwa katika soka ya Ujerumani. Bao lililowavunia Bayern alama tatu katika gozi dhidi ya Dortmund lilifumwa wavuni na Joshua Kimmich aliyemwacha hoi kipa Roman Burki kunako dakika ya 43. Baada ya kuonekana kuzidiwa maarifa katika takriban kila idara, Dortmund walilazimika kumleta ugani chipukizi Jadon Sancho katika kipindi cha pili ila ujio wake haukutosha kuwarejesha waajiri wake mchezoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako