• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Dodoma FC kuanza mazoezi Alhamis

    (GMT+08:00) 2020-05-27 15:47:45

    Uongozi wa timu ya Dodoma FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) umepanga kikosi chao kuanza mazoezi rasmi kesho kujiandaa na mechi zao zilizosalia. Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mbwana Makata kitaingia kambini Mei 27 ambapo wachezaji wote wanapaswa kuwepo kwa ajili ya mpango wa mazoezi ambao itawawezesha kujiimarisha zaidi kabla ya kuelekea Mwanza ambapo ndicho kituo kinachotumika kwa ajili ya mechi za FDL na Daraja la Pili (SDL). Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Fortunatus John amesema kuwa, timu itaingia kambini ikiwa na matumaini makubwa na ari ya mazoezi kwa lengo la kuivusha timu hiyo kutoka FDL kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) msimu ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako