• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Bigirimana kutua Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2020-05-27 15:48:02

    Mshambuliaji wa klabu ya Namungo FC raia wa Burundi Bigirimana Blaise, ambaye amekuwa na kiwango bora katika msimu huu wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara, amesema meneja wake wamepokea ofa kutoka Afrika Kusini. Awali Bigirimana ambaye msimu huu ametoa mchango mkubwa wa ushindi kwenye klabu ya Namungo FC, alihusishwa kujiunga na Young Africans akiwa mwishoni mwa mkataba wake, lakini pia timu kutoka Africa Kusini imeona uwezo wake na kuhitaji kumsajili nyota huyo. Mshambuliaji huyo amesema ni kweli kwamba timu ya Yanga walizungumza naye wakitaka ajiunge na timu hiyo, na pia kuna timu moja ya nchini Afrika Kusini ambayo pia inamtaka. Hata hivyo uongozi wa Namungo FC bado unadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na mshambuliaji huyo, kufuatia mkataba wake kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako