• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wa Bunge la Umma la China wajadili mswada wa Mkusanyiko wa sheria za kiraia

    (GMT+08:00) 2020-05-27 17:16:48

    Wajumbe wa Bunge la Umma la China wamejadili mswada wa kwanza wa mkusanyiko wa sheria za kiraia wa China, na wanaona kuwa, mswada huo umeonesha umaalumu wa kipekee wa China, umaalumu wa zama za sasa, na nia ya wananchi. Wajumbe hao wanaona kuwa, vifungu vilivyowekwa kwenye mswada huo vina umuhimu mkubwa katika kulinda vizuri zaidi haki za wananchi na kuhimiza watu kupata maendeleo kwa pande zote.

    Kiini cha mswada huo ni kulinda kwa pande zote haki za wananchi, na "Haki ya nafsi ya mtu" inafuatiliwa zaidi. Mjumbe wa Bunge la Umma la China ambaye pia ni mkurugenzi wa Mkutano wa Washiriki wa Ofisi ya wanasheria ya Hua Ju ya mkoa wa Shanxi Bw. Liu Zheng anaona kuwa, mswada huo unasisitiza kulinda nafsi na heshima ya wananchi, hali ambayo imeonesha wazo la maendeleo la kutoa kipaumbele wananchi. Mswada huo pia umeweka bayana kupiga marufuku vitendo vya kudhuru maisha binafsi ya watu kwa njia yoyote ikiwemo ya simu, ujumbe mfupi, barua pepe. Anaona kuwa sheria hiyo inalinda kwa ufanisi faragha kwa wananchi. Anasema:

    "Kuweka vifungu maalumu kuhusu haki ya nafsi ya mtu, na kuhusisha utekelezaji wa kuhakikisha nafsi na heshima ya wananchi kutoathiriwa kwenye katiba, kumeonesha uthibitishaji na ulinzi wa haki ya nafsi ya wananchi."

    Mjumbe mwingine wa Bunge hilo ambaye pia ni Mkuu wa Shirikisho la Wanasheria la Mkoa wa Guangdong Bw. Xiao Shengfang anaona kuwa, mkusanyiko huo ni azimio la haki za wananchi. Amezungumzia majukumu yaliyothibitishwa kwenye mkusanyiko huo ambayo yanahusisha pande mbalimbali zinazotakiwa kuwajibika na kitendo cha "kuangusha vitu kutoka jengo lenye ghorofa ya juu", akisema kuwa kifungu hicho kinalinda kwa hatua zenye ufanisi usalama wa wananchi. Anasema:

    "Katika miaka ya hivi karibuni, matukio ya kuangusha vitu kutoka jengo lenye ghorofa ya juu yametokea mara kwa mara. Mswada huo umeweka kanuni bayana kuwachunguza kwa wakati kwa watu wanawajibika na vitendo hivyo. Kampuni inayoshughulikia utoaji wa huduma kwa mitaa ya makazi pia inatakiwa kuchukua hatua za lazima kulinda usalama wa wakazi."

    Mbali na hayo, mswada huo umeimarisha ulinzi wa usalama kwa data za mtandao wa Internet, na kukubali hadhi ya kisheria ya mali zisizo halisi ambazo zilipatikana kwenye mtandao wa Internet. Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni mkuu wa Shirikisho la wanasheria la mji wa Beijing Bw. Gao Zicheng anaona kuwa, hizi ni kanuni mpya zinazotolewa kutokana na hali mpya na masuala mapya zinazoibuka katika maisha ya kijamii na kiuchumi. Anasema:

    "Mswada huo vilevile unahusisha vifungu vya kulinda usalama wa data kubwa na mali zisizo halisi ambazo zinapatikana na kutumika kwenye mtandao wa Internet, ambao umeweka vigezo vya pamoja kwa ajili ya utekelezaji wa sheria katika siku za mbele."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako