• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa tatu wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China wafungwa

    (GMT+08:00) 2020-05-27 19:50:17

    Mkutano wa tatu wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China umefungwa hapa Beijing baada ya kumaliza kujadili ajenda mbalimbali, na viongozi wa chama cha kikomunisiti cha China CPC na nchi akiwemo rais Xi Jinping wa China wamehudhuria ufungaji wa mkutano huo.

    Mkutano huo umepitisha uamuzi kuhusu ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya Baraza hilo, ripoti kuhusu hali ya ukaguzi wa mapendekezo na azimio la kisiasa la mkutano.

    Akihutubia ufungaji wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Wang Yang amesema, Baraza hilo lililo chini ya Chama cha Kikomunisti cha China linatakiwa kutumia nguvu bora ya mashauriano ya kiujamaa, kushirikisha kwa ufanisi vyama mbalimbali vya kisiasa na watu kutoka hali mbalimbali katika kujadili masuala ya kitaifa, kutoa mapendekezo na kufikia makubaliano ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako