• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikutano Miwili ya kisiasa nchini China yatoa kipaumbele katika masuala mambo yanayohusiana na wananchi

    (GMT+08:00) 2020-05-28 17:28:04

    Tangu mkutano mkuu wa Kamati Kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika, rais Xi Jinping ametoa umuhimu mkubwa kwa "matumaini ya wananchi kuwa na maisha mazuri" kuwa lengo la utawala wa Chama cha Kikomunisti cha China. Wakati wa Mikutano Miwili ya mwaka huu inayofanyika wakati China ikikabiliana na janga la virusi vya Corona, rais Xi Jinping alizungumza na wajumbe waliohudhuria mikutano, na alitoa umuhimu mkubwa katika mambo yanayohusiana na wananchi.

    Katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Bunge la Umma la China mwaka huu, Rais Xi alijadiliana na wajumbe kutoka mkoa wa Mongolia ya Ndani kuhusu ripoti ya kazi ya serikali, aliuliza mara nyingi jinsi gani hali ya uchumi iliathiriwa kutokana na virusi vya Corona.

    Tangu janga hilo ilipoibuka nchini China, rais Xi Jinping amechukua nafasi ya uongozi na kuweka mipango kuhusu kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi, na kufanya mikutano kadhaa ya wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama, Mikutano mitano na Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu, kufanya ziara za ukaguzi mara sita katika mikoa mbalimbali, na mazungumzo zaidi ya 50 na viongozi wa nchi za nje na wakuu wa Mashirika ya Kimataifa kwa njia ya simu au video. Hata hivyo aliwauliza hali halisi alipokutana na wajumbe hao ana kwa ana.

    Ili kukabiliana na changamoto ya janga la virusi vya Corona, "kutoa kipaumbele wananchi" ni wazo analoshikilia rais Xi Jinping siku zote. Anasema:

    "Kutoa kipaumbele kwa wananchi, na kutoa kipaumbele kwa maisha. Kulinda usalama wa maisha na afya ya wananchi kadiri iwezekanavyo."

    Rais Xi amesisitiza kuwa, inapaswa kutegemea vizuri wananchi, na kutatua masuala wanayoyafuatilia ikiwemo nafasi za ajira, elimu, bima ya kijamii, matibabu, nyumba na utunzaji wa uzeeni.

    "Uti wa mgongo wa Chama cha kikomunisti cha China unatokana na wananchi. Inapaswa kushikilia wazo la kujiendeleza kwa kutoa kipaumbele kwa wananchi, na halipaswi kubadilika bila ya kujali linakabiliwa na changamoto na shinikizo gani, au kupata hasara kubwa kiasi gani."

    Wakati wa mikutano hiyo, rais Xi pia amefuatilia maslahi ya wakulima. Mwaka huu wa 2020, China si kama tu itajitahidi kushinda mapambano dhidi ya virusi vya Corona, bali pia itatimiza lengo la kutokomeza umaskini, na kuhimiza mambo ya kisasa ya kilimo chini ya hali mpya, ili kuwafanya wakulima wapate utajiri kama wakazi wa mijini. Anasema:

    "Watu wa umri kama wangu tuna matumaini ya kuwasaidia wakulima. Njia ya kutimiza ujamaa haitaacha mtu hata mmoja, na ni lazima tupate utajiri kwa pamoja."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako