Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amekutana na wanahabari baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Bunge la Umma la China.
Katika mkutano huo, Li Keqiang amesema, China haijaweka lengo la ongezeko lapato la taifa, lakini imeweka malengo ya kuhakikisha utoaji wa nafasi za ajira, maisha ya msingi ya watu na ushiriki wa soko, ambayo yatawafanya wananchi kuhisi ukuaji wa uchumi na kulifanya ongezeko la uchumi kuwa na sifa ya juu zaidi.
Amesema, China inapenda kuendelea kufanya ushirikiano wa kimataifa, ili kushinda kwa pamoja virusi vya Corona. Hivi sasa jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na changamoto za kudhibiti maambukizi na kurejesha maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hivyo ni wakati mwafaka wa kufanya ushirikiano wa kimataifa.
Pia ameahidi kuwa fedha zinazotengwa na serikali ya China kwa lengo la kukabiliana na matatizo yanayotokana na athari za maambukizi zitatumiwa katika maisha ya msingi ya watu.
Aidha, Bw. Li amesisitiza kuwa katika msingi wa kanuni ya "Kuwepo kwa China Moja", makubaliano ya mwaka 1992 na kupinga kithabiti jaribio la kuifanya Taiwan ijitenge kutoka China, serikali ya China inapenda kufanya juhudi kubwa na kwa udhati zaidi kufanya mazungumzo na vyama mbalimbali vya kisiasa, makundi na watu wa hali mbalimbali wa Taiwan, ili kuhimiza maendeleo ya amani kati ya kando mbili za Mlango Bahari wa Taiwan na umoja wa taifa kwa njia ya amani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |