• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FIFA yafafanua adhabu ya kutemna mate uwanjani

    (GMT+08:00) 2020-05-29 08:37:30

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limetoa muongozo kwa vyama na mashirikisho ya soka duniani kuwa na uamuzi binafsi juu ya adhabu ya kutema mate katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona. Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya FIFA, Pierluigi Collina katika barua yake kwa vyama na mashirikisho ya soka, amesema kuwa kamati hiyo haina mamlaka ya moja kwa moja juu ya adhabu kutokana na kosa hilo kufuatia mapendekezo yaliyotolewa hivi karibuni. Kutokana na tatizo la virusi vya Corona, kundi kubwa la wadau wa soka limependekeza kuwa kosa la kutema mate liwe la kadi nyekundu iwe kwa mchezaji kumfanyia mwenzake au kutema popote pale uwanjani. Ligi mbalimbali zimeanza kurejea duniani baada ya kusimama tangu mwezi Machi, ikiwa ni miongoni mwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kukabiliana na virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako