• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Brescia wajuta kumsajili Mario Balotelli

    (GMT+08:00) 2020-05-29 15:55:36

    Mmiliki wa kikosi cha Brescia kinachoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Massimo Cellino, amesema kwamba anajutia sana hatua ya kuwahi kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool, Mario Balotelli. Tangu aingie katika sajili rasmi ya Brescia mwanzoni mwa msimu huu, Balotelli, 29, ambaye ni mzawa wa Italia, amefunga jumla ya mabao matano akiwa mchezaji wa kikosi hicho. Hata hivyo, Cellino amesema kwamba Balotelli kwa sasa yuko huru kuondoka kambini mwa Brescia ambao wananing'inia pembamba mkiani mwa jedwali la Serie A kwa alama 16 kutokana na jumla ya michuano 26 iliyopita. Amesema tatizo kubwa la Balotelli ni kwamba anakosa vipindi vya mazoezi, hawajibikii kikosi kwa kujituma ipasavyo na hana maazimio yoyote yanayohusiana na maendeleo ya klabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako