• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mwenyekiti wa Arsenal Sir Chips Keswick astaafu

    (GMT+08:00) 2020-05-29 16:04:46

    Sir Chips Keswick amestaafu kwenye uenyekiti wa Arsenal baada kuhudumu katika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka saba. Kinara huyo mwenye umri wa miaka 80 ambaye pia ni shabiki sugu wa tangu zamani wa Arsenal, amekuwa kwenye bodi ya usimamizi wa Arsenal tangu mwaka 2005 na akateuliwa kuwa Mwenyekiti mwaka 2013 baada ya kuaminiwa kuwa mrithi wa Peter Hill-Wood. Arsenal wamesema hawawazii kwa sasa kujaza pengo la Keswick hasa ikizingatiwa ukubwa wa uwezo unaojivuniwa na wanachama wao wa sasa kwenye bodi ya usimamizi wakiwemo Stan na Josh Kroenke, Lord Harris na Ken Friar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako