• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Timu ya Wanawake ya Manchester City yamteua Gareth Taylor awe kocha wao

    (GMT+08:00) 2020-05-29 16:05:08

    Timu ya soka ya wanawake ya Manchester City imemteua mshambuliaji matata wa zamani wa timu ya taifa ya Wales, Gareth Taylor kuwa kocha mpya kwa mkataba wa miaka mitatu. Taylor, 47, aliwahi kuvalia jezi za Man-City kati ya 1998 na 2001. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa akiongoza akademia ya wavulana wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza. Uteuzi wake ulichochewa na ulazima wa kujazwa kwa pengo la Nick Cushing aliyeagana na Man-City mnamo Februari 2020 kwa minajili ya kuwa kocha msaidizi wa kikosi cha New York City kinachoshiriki Major League Soccer (MLS) nchini Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako