• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ajibu barua iliyoandikwa na wanasayansi na wafanyakazi wa teknolojia

    (GMT+08:00) 2020-05-29 16:45:57

    Rais Xi Jinping wa China leo amewataka wafanyakazi katika sekta ya sayansi na teknolojia kutoa mchango mpya na mkubwa katika kuijenga China kuwa na nguvu kubwa katika sayansi na teknolojia.

    Rais Xi amesema hayo alipokuwa akijibu barua iliyoandikwa na wawakilishi wa wafanyakazi hao, na kuwataka kuongeza juhudi ili kutimiza mafanikio katika teknolojia muhimu. Rais Xi amesema, wafanyakazi wengi katika sekta ya sayansi na teknolojia wamejitolea kuhudumia nchi kupitia mawazo na vitendo vyao vya kiuvumbuzi.

    Rais Xi amesema, uvumbuzi ni kichocheo muhimu cha msingi katika maendeleo, na sayansi na teknolojia ni zana muhimu katika kukabiliana na changamoto.

    Amesema katika kukabiliana na mlipuko wa ghafla wa virusi vya Corona, wafanyakazi wa sekta hiyo walikabiliana na changamoto na kufanya kazi bila kuchoka katika tiba, utafiti wa chanjo, maendeleo, na matumizi ya data kubwa, hivyo kutoa uungaji mkono wa kisayansi na teknolojia katika kupambana na virusi hivyo.

    Rais Xi ametumia nafasi hiyo kutoa salamu kwa wafanyakazi wote wa sekta ya sayansi na teknolojia nchini China, kabla ya Siku ya Nne ya Kitaifa ya Wafanyakazi wa Sekta ya Sayansi na Teknolojia, inayoangukia Mei 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako