• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mwandamizi wa Zimbabwe asisitiza sheria ya Hongkong inasaidia mshikamano na maendeleo ya China

    (GMT+08:00) 2020-05-29 18:34:54
    Waziri wa Habari na Utangazaji wa Zimbabwe Bi Monica Mutsvangwa hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, alisisitiza kuwa Hongkong ni sehemu isiyoweza kutengeka ya China, na utungaji wa sheria inayohusu usalama wa taifa wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hongkong unasaidia mshikamano na maendeleo ya China.
    Bibi Mutsvangwa pia amesema, sheria hiyo ni jibu lenye nguvu kwa nguvu za nje kuingilia kati mambo ya ndani ya China. Anasema:
    "Hatua ya serikali kuu ya China kuhusu mambo ya Hongkong inalenga kulinda muungano wa nchi. Nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya hali ya Hongkong, vitendo vinavyokwenda kinyume cha sheria ambavyo vilitokea kwenye vurugu haviwezi kuvumiliwa. Nafurahia serikali ya China kufanya juhudi katika kutatua suala hilo, na kuchukua hatua za kumaliza vitendo vinavyojaribu kufarakanisha nchi."
    Pia ameeleza kuwa, maendeleo ya nchi hayawezi kupatikana bila ya amani na mshikamano. China kuanzisha na kukamilisha sheria ya kulinda usalama wa nchi kwenye mkoa wa Hongkong kutasaidia umoja na maendeleo ya nchi. Anasema:
    "China ikiwa nchi yenye mamlaka kamili, inafahamu namna ya kulinda maslahi ya wananchi wake, kuunganisha watu wote nchini, na namna ya kuendeleza uchumi. Ni nchi yenye amani na mshikamano itakayoweza kupata maendeleo. Ndiyo maana tunaiunga mkono China kuanzisha na kukamilisha sheria ya Hongkong kuhusu kulinda usalama wa nchi, pia tunatumaini kuwa nguvu za nje zinazojaribu kuzusha vurugu, kuifarakanisha China na kudhuru maendeleo ya uchumi ya China zitaacha vitendo vyao."
    Akizungumzia Mikutano Miwili iliyofanyika nchini China, Bi Mutsvangwa amesema mafanikio ya mikutano hiyo na sera mbalimbali zilizotangazwa, zitachangia katika kutuliza uchumi wa dunia. Amesema ana matumaini makubwa juu ya uchumi wa China. Akisema:
    "Maambukizi ya virusi vya Corona yameleta athari kubwa kwa uchumi wa dunia ikiwemo China. China imechukua hatua kwa wakati na zenye ufanisi katika kukabiliana na janga hili, na kufanikiwa kuzuia kuenea kwa virusi hivyo. Hivi sasa mji wa Wuhan umefunguliwa tena, uchumi umeanza kufufuka, hali iliyoonesha kwa dunia kuwa binadamu atashinda katika mapambano dhidi ya virusi hivyo. Najua wananchi wa China wamefanya juhudi kubwa, na kupata maendeleo makubwa. Nina matumaini makubwa juu ya uchumi wa China."
    Bi Mutsvangwa vilevile anaona kuwa Mikutano hiyo imeonesha nia na imani ya China katika kutimiza lengo la kutokomeza umaskini. Akisema:
    "Mafanikio ya China katika kupunguza umaskini yanafuatiliwa na watu duniani. Mimi pia nimeshuhudia juhudi hizo za China. Mwaka 2002 nilipowasili Beijing kuanza kazi yangu niliona watu maskini kwenye sehemu kadhaa nchini China, lakini nilipoondoka China baada ya miaka mitano, China ilikuwa imepata mabadiliko makubwa. Hivi sasa mchakato wa China katika kupunguza umaskini unaendelea kwa kasi na kuwa na ufanisi mkubwa."
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako